Scholz asisitiza kuhusu mazungumzo ya amani kwa Ukraine
8 Septemba 2024Matangazo
Katika mahojiano yaliyorushwa kwa njia ya televisheni, Scholz amekiambia kituo cha ZDF kwamba anaamini sasa ndio wakati wa kujadili jinsi ya kufikia amani katika hali ya sasa ya vita kwa kasi ya juu.
Soma pia.Scholz akiri matokeo yaliyokipa ushindi chama cha AfD yanatia wasiwasi
Scholz anakabiliwa na shinikizo nchini mwake baada ya vyama vyote vitatu katika muungano wake wa mrengo wa kati kushindwa kwenye uchaguzi katika majimbo mawili wiki moja iliyopita, hukuvyama vinavyotafuta mahusiano bora na Urusi yakipata kura zaidi.
Chama cha mrengo wa kulia Alternative for Germany, AfD, na kingine kipya cha upinzani, BSW, vinavyopinga msaada wa kijeshi kwa Ukraine katika vita vyake na Urusi, vyote vimepata mafanikio makubwa kwenye uchaguzi huo.