Zelensky amfuta kazi mkuu wa majeshi
9 Februari 2024Matangazo
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov aliyasema hayo siku ya Alkhamis (Februari 8) na kulingana na Zelensky, utawala mpya umeanza kazi mara baada ya uteuzi.
Tangu mwishoni mwa mwaka uliopita, vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti juu ya kutoelewana kati ya Zelensky na Zaluzhnyi.
Soma zaidi: Rais Putin asema hawana maslahi nchini Poland wala Latvia
Siku ya Akkhamis, Zelensky aliandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba amekutana na Zaluzhnyi na kumweleza juu ya hatua hiyo na kujadiliana juu ya mabadiliko yanayohitajika ndani ya jeshi na mtu anayefaa kuchukua nafasi hiyo.
Kulingana na Zelensky, Zaluzhnyi atasalia kwenye timu inayoongoza mapambano dhidi ya uvamizi wa Urusi.