Zelenskiy akutana na Papa Francis
11 Oktoba 2024Matangazo
Mkutano wa Zelensky Vatican City ni sehemu ya ziara yake ya kuzunguka miji mikuu ya nchi za Ulaya akilenga kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa washirika wake kabla ya majira ya baridi kali.
Leo alasiri amekutana na Kansela Olaf Scholz mjini Berlin ambako, kiongozi huyo wa Ujerumani ameahidi kuipa Kiev msaada wa ziada wa silaha wa dola bilioni 1.5.
"Huu ni ujumbe wa wazi kwa Putin. Mchezo wa kuburuza muda ni hatua ambayo haitofanikiwa. Hatuwezi kuacha kuisadia Ukraine,'' alisema Scholz.
Zelensky anatafuta msaada zaidi wa kijeshi na kifedha katika ziara yake ya saa 48 London, Paris, Rome na Berlin, katikati ya kiwingu cha khofu ya kusitishwa msaada huo, ikiwa Donald Trump atashinda uchaguzi wa rais nchini Marekani mwezi ujao wa Novemba.