Zaidi ya watoto milioni 20 hawakupewa chanjo ya surua
25 Aprili 2019Matangazo
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwashughulikia Watoto - UNICEF imetaja kuwa miripuko ya ugonjwa wa surua tunayoiona sasa ilisababishwa na ukosefu wa chanjo katika miaka ya nyuma. UNICEF imekadiria kuwa watoto milioni 169 walikosa chanjo ya kwanza ya surua kati ya mwaka wa 2010 na 2017 - ikiwa ni idadi ya wastani ya watoto milioni 21.1 kila mwaka. Matokeo yake ni kuwa maambukizi ya surua kote duniani yaliongezeka karibu mara nne katika robo ya kwanza ya mwaka wa 2019 ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho katika mwaka wa 2018 kufikia idadi ya watoto 112,163. Surua ni ugonjwa unaombukiza sana ambao unaweza kuuwa na kumfanya mtu kutoweza kuona, kusikia au maradhi ya ubongo.