1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya wahamiaji 500 waokolewa katika visiwa vya Canary

6 Juni 2024

Mamia ya wahamiaji waliokuwa katika hali ya dharura wameokolewa karibu na visiwa vya Canary nchini Uhispania.

https://p.dw.com/p/4gkID
Wahamiaji wasafiri katika bahari ya Mediterania
Wahamiaji hufunga safari hatari ndani ya boti na kujaribu kuvuka bahari ya Mediterania wakitaka kufika UlayaPicha: Europa Press/ABACA/picture alliance

Idara ya dharura ya nchi hiyo zimesema timu za uokoaji zilifanya kazi usiku kucha ili kuwanusuru jumla ya wahamiaji 516.

Soma pia: Idadi ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka bahari ya Mediterania kuelekea Ulaya yaongezeka

Wahamiaji hao waliokuwa wakisafiri ndani ya boti tano ni pamoja na vijana na watoto, wengi wao wakitokea hasa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Soma pia: UN yaonya kuhusu sera ya uhamiaji ya nchi za Ulaya

Abiria waliwaambia waokoaji kuwa watu wasiopungua kumi walikufa kwenye moja ya boti na miili ilitupwa baharini.

Vyombo vya habari vya Uhispania viliripoti kwamba mwanamke mmoja alijifungua akiwa kwenye boti.

Watu hao, wengine wakiwa katika hali mbaya, walipelekwa kwenye maeneo ya karibu na kisiwa cha Canary.