1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaonya kuhusu sera ya uhamiaji ya nchi za Ulaya

4 Juni 2024

Mjumbe maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ameonya kuhusu hatari ya mparaganyiko iwapo Ulaya itachukua msimamo mkali zaidi dhidi ya wahamiaji baada ya uchaguzi ujao wa Bunge la Ulaya.

https://p.dw.com/p/4gdna
Mjumbe maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Vincent Cochetel
Mjumbe maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Vincent CochetelPicha: Martial Trezzini/KEYSTONE/picture alliance

Vincent Cochetel, mjumbe katika eneo la kati na magharibi mwa Mediterania, amesema hatua kama hiyo ya Ulaya ambayo imekuwa ikichukuliwa kama mfano wa kuigwa, inaweza kuathiri utayari wa nchi nyingine duniani kuwapokea wahamiaji.

Soma pia:Ujerumani: Wafuasi wa chama kipya cha siasa BSW waipinga AFD

Cochetel amesema jambo hilo linaweza pia kupelekea nchi ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikiwapa hifadhi watu wanaokimbia machafuko, kufikiria upya sera zao. Kwa miaka kadhaa sasa nchi nyingi za Ulaya zimekuwa zikijaribu kuwa na sera kali dhidi ya uhamiaji.