Yemen: Waasi waonyesha matumaini baada ya mazungumzo
20 Septemba 2023Mapema leo, Riyadh imesifu matokeo chanya kwenye mazungumzo hayo na waasi ingawa haikutoa maelezo ya kina ya majadiliano hayo yanayolenga kuhitimisha vita vinavyoigharimu pakubwa Yemen.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia imekaribisha matokeo hayo chanya yanayolenga kuanzishwa mkakati madhubuti wa kuunga mkono upatikanaji wa amani nchini humo.
Waasi hao wametoa masharti ambayo ni pamoja na watumishi wa umma wa Houthi kulipwa mishahara, kuachiwa kwa wafungwa wa Houthi na kuanzishwa kwa njia mpya kutokea uwanja wa ndege wa Sanaa unaodhibitiwa na Houthi.
Mazungumzo haya ni ishara ya karibuni zaidi inayoibvua matumaini mapya tangu Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ulipoivamia Yemen kijeshi mwaka 2015.
Soman Pia:
Saudia yasifu "matokeo chanya" ya mazungumzo na waasi wa Houthi wa Yemen