1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaAsia

Kisa cha maambukizi ya mafua ya ndege chagundulika India

12 Juni 2024

Shirika la Afya Duniani WHO limegundua kisa cha maambukizi ya homa ya mafua ya ndege kwa mtoto wa miaka minne inayosababishwa na virusi aina ya H9N2 huko katika jimbo la West Bengal nchini India.

https://p.dw.com/p/4gw9E
Wanyama wa shambani wanaofugwa kwenye vizimba | kuku wa mayai
Eneo la ufugaji wa kuku Aprili 18, 2013 huko Liaocheng, Mkoa wa Shandong nchini China. Picha: China Foto Press/IMAGO

Mgonjwa alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na hali mbaya iliyomkabili katika mfumo wake wa upumuaji, homa kali na maumivu ya tumbo mwezi Februari, na aliruhusiwa miezi mitatu baadae baada ya kupata matibabu. Inaelezwa mgonjwa huyo alitokea katika mazingira ambayo yanafugwa kuku nyumbani kwao na hapakuwa na mtu anayejulikana aliyeripoti dalili za ugonjwa wa kupumua kati ya familia yake na mawasiliano mengine.WHO iliongeza kwa kusema taarifa juu ya hali ya chanjo na maelezo ya matibabu ya kukabiliana na virusi hayakupatikana wakati mgonjwa alipowasilishwa hospitali. Haya ni maambukizi ya pili ya binadamu ya mafua ya ndege ya virusi aina ya H9N2 kutoka India, ya kwanza yalitokea  2019.