SiasaMexico
WHO: Mtu wa kwanza kuambukizwa virusi vya H5N2 afariki
8 Juni 2024Matangazo
Wizara ya Afya ya Mexico ilisema mtu huyo mwenye miaka 59 alikuwa pia na historia na maradhi sugu ya figo, kisukari na shinikizo la damu la muda mrefu.
WHO siku ya Jumatano lilitangaza kwamba kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya H5N2 avian kwa mwanadamu kiliripotiwa nchini Mexico.
Alilazwa kwa wiki tatu na mnamo Aprili 7, aligundulika kuwa na dalili za homa kali, kukosa pumzi, kuharisha, kichefuchefu na kwa ujumla kujisikia vibaya.
Msemaji wa WHO Christian Lindmeier amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba pamoja na dalili hizo, vipimo vya mgonjwa huyo vilionyesha kuambikizwa virusi hivyo vya H5N2 na uchunguzi wa namna alivyoambukizwa unaendelea.