WHO yaomba msaada wa haraka wa vifaa tiba Gaza
12 Septemba 2024Kulingana na tathmini ya WHO, mahitaji makubwa ya matibabu, sehemu za bandia za mwili na vifaa vya kusaidia kutembea havipatikani vya kutosha.
Mwakilishi wa Shirika la Afya katika Ukanda wa Gaza, Richard Peeperkorn, amesema wanahitaji msaada kwa haraka hasa vifaa tiba vya kukarabati miili ya watu na kwamba hawawezi kusubiri mpaka makubaliano ya kusimamisha vita yatakapofikiwa.
Soma pia:Watu 18 wameuwawa baada ya Israel kushambulia shule katikati mwa Ukanda wa Gaza
WHO, imesema wagonjwa wengi wanaohitaji ukarabati wameumia viungo na kwamba kati ya watu 3000 hadi 4000 wamekatwa viungo tangu vita vilipoanza katika Ukanda wa Gaza. Kulingana na shirika hilo, tatizo hilo la uhaba wa vifaa tiba muhimu na madaktari ni mambo yanayoongeza shida kwa watu wa Gaza.