WHO: Afrika ina barabara, gari chache lakini ajali nyingi
2 Oktoba 2024Ripoti hiyo ya hivi karibuni ya WHO inasema ajali hizo zinachochewa na uzembe, mwendo mkali, ulevi, miundombinu mibovu na magari mabovu.
Wataalamu wanasema maeneo mengine pia yanakabiliwa na changamoto kama hizo na nyingine kama za kutofunga mikanda ama kutovaa kofia ngumu.
Soma zaidi: Watu 32 wapoteza maisha ajali ya barabarani Misri
Lakini kwa Afrika, ambako vifo 620 vya barabarani hutokea kila siku, hali huwa ni mbaya zaidi kutokana na barabara mbaya, magari makuukuu na upungufu wa huduma za dharura.
Ripoti hiyo ya WHO inasema Afrika imelitangulia eneo la kusini mashariki mwa Asia kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo vya barabarani vya wastani wa watu 19.5 kati ya 100,000 kwa mwaka 2021.
Mwaka uliopita, Afrika - yenye asilimia 4 tu ya magari yote ulimwenguni - ilikabiliwa na asilimia 19 ya vifo vyote vya barabarani ulimwenguni.