1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WFP inahitaji dola milioni 400 kuwalisha watu Barani Afrika

22 Mei 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula limesema linahitaji dola milioni 400 kuwalisha mamilioni ya watu wanaohitaji msaada wa chakula katika mataifa ya Kusini mwa Afrika yanayokabiliwa na ukame na njaa.

https://p.dw.com/p/4g9Wo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, usambazaji wa chakula katika kambi ya wakimbizi ya Shasha
Usambazaji wa chakula katika kambi ya wakimbizi ya Shasha huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Trappe/Caro/picture alliance

Shirika hilo la WFP limewaambia waandishi habari leo Jumatano kwamba linahitaji haraka fedha za kusimamia msaada wa miezi sita kuzisaidia Zimbabwe, Zambia na Malawi ambazo zimepungukiwa na mavuno ya chakula kufuatia hali ya hewa ya El Nino iliyosababisha ukame. Watu milioni 4.8 wameathirika.

Msemaji wa WFP  Tomson Phiri  amesema takriban asilimia 70 ya watu katika kanda hiyo ya Kusini mwa Afrika  ambao wanategemea mvua kwaajili ya kilimo wamekosa mavuno kutokana na ukosefu wa mvua.