Waziri wa nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, yupo Slovenia
5 Desemba 2023Matangazo
Pamoja na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Kabla ya kuwasili Slovenia waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani, alibaini kwamba mapambano dhidi ya mgogoro wa mabadiliko ya tabia nchi ni kitisho kikubwa kwa usalama wa binadamu na kwamba utekelezaji wa mpango kati ya Ujerumani na Slovenia utaanza kwa kulitazama hilo. Baadae Baerbock ambaye ni mwanasiasa wa chama cha kijani nchini Ujerumani, amepangiwa kukutana na waziri mkuu Robert Golob na waziri wa mambo ya nje Tanja Fajon katika mji mkuu wa Slovenia, Ljubljana. Mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita zaidi katika suala la kuzijumuisha nchi za Balkan katika Umoja wa Ulaya kufuatia vita vya Urusi na Ukraine.