Baerbock aonya kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi
16 Novemba 2023Wito huo wa Baerbock uliotolewa jana Jumatano, unakuja takriban wiki mbili kabla ya kongamano la kimataifa la Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP 28 huko Dubai. Baerbock ameonya dhidi ya kupuuza vita dhidi ya ongezeko la joto duniani na athari zake mbaya . Baerbock amesema kuwa mzozo wa hali ya hewa hautambui mabomu na makombora lakini unaathiri kila mmoja bila huruma.
Mfuko kutumika kufidia athari za ongezeko la joto duniani
Mfuko huo, uliokubaliwa wakati wa mkutano wa hali ya hewa wa mwaka jana, unapaswa kutumika kutoa misaada baada ya matukio mabaya ya hali mbaya ya hewa yaliosababishwa na ongezeko la joto duniani, kama vile dhoruba au ukame.
Hata hivyo, kwa mujibu wa pendekezo la maelewano ya muda, takriban mataifa hayo 200 yatakaowakilishwa katika mkutano huo wa COP28, yatachangia kwa hiari katika mfuko huo wakati ambapo hakujakubaliwa kiwango maalumu.