1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Waziri wa mambo ya nje wa Iran ziarani Marekani

26 Oktoba 2023

Iran imesema Amirabdollahian aliwasili New York usiku wa kuamkia leo kwa lengo la kuyaunga mkono maslahi ya Palestina katika mkutano wa Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4Y3Bg
Waziri wa mamabo ya nje waIran Hossein Amirabdollahian
Waziri wa mamabo ya nje waIran Hossein Amirabdollahian Picha: Hassan Ammar/AP Photo/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hussein Amirabdollahian amefanya ziara ya ghafla kuelekea Marekani iliyochochewa na mzozo wa Gaza.

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema Amirabdollahian aliwasili New York usiku wa kuamkia leo kwa lengo la kuyaunga mkono maslahi ya Palestina katika mkutano wa Umoja wa Mataifa. Ziara za maafisa wa ngazi ya juu wa Iran nchini Marekani ni nadra mno kwa kuwa Jamhuri hiyo ya Kiislamu inaichukulia Marekani kama adui wake mkubwa.

Israel imeushambulia Ukanda wa Gaza kwa mabomu tangu wanamgambo wa Hamas kufanya mauaji ya Waisraeli 1,400 mnamo Oktoba 7.