SiasaUrusi
Lavrov ahudhuria mkutano wa Caucasus nchini Iran
24 Oktoba 2023Matangazo
Sergei Lavrov pia alifanya mazungumzo tofauti na waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hussein Amirabdollahian. Mkutano huo wa ngazi ya mawaziri ulilenga kuzijumuisha jamhuri tatu za zamani za muungano wa zamani wa Sovieti katika eneo la Caucusus, zikiwamo Armenia, Azerbaijan na Georgia, pamoja na dola kubwa jirani - Urusi, Uturuki na Iran.
Georgia iliamua kutoshiriki mkutano huo wa pande sita. Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni hali kufuatia harakati za Azerbaijan katika eneo la Nagorno-Karabakh na kutimuliwa kwa Warmenia kutoka eneo hilo. Mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia haujatatuliwa kikamilifu.