1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annalena Baerbock atoa wito wa suluhisho la mataifa mawili

10 Novemba 2023

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, amezitolea wito mataifa ya kiarabu ya eneo la Ghuba kuunga mkono mataifa mawili kama suluhisho la vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas.

https://p.dw.com/p/4YgPl
Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Annalena BaerbockPicha: Sina Schuldt/dpa/picture alliance

Baerbock ametoa wito huo kabla ya ziara yake kuelekea Umoja wa falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Israel, ambapo amesisitiza kuwa kutimizwa kwa ahadi ya kuwa na mataifa mawili ndiyo njia pekee ya amani, usalama na heshima ya kudumu kwa Israel na Wapalestina.

Israel kuanza usitishaji vita kwa masaa manne kila siku Gaza

Annalena Baerbock ameongeza kuwa kuhakikisha mateka wanaachiliwa, kutanua juhudi za kuwafikishia wahanga wa vita misaada ya kiutu huko Gaza na kumaliza vita kote katika kanda hiyo vinaweza kufaulu tu ikiwa watashirikiana na mataifa yote ya Ghuba.