1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kuanza usitishaji vita kwa masaa manne kila siku Gaza

10 Novemba 2023

Israel inatarajiwa kuanza mpango wa usitishaji vita kwa saa nne kila siku katika maeneo ya kaskazini mwa Gaza ili kuruhusu raia kuondoka maeneo hatari.

https://p.dw.com/p/4Yetp
Deutschland Pro-Palästina-Demo in Berlin
Picha: Andreas Friedrichs/IMAGO

Marekani imetangaza hayo kupitia msemaji wa Baraza la Usalama wa Kitaifa John Kirby, aliyetaja hatua hiyo kuwa “mwelekeo sahihi”.

John Kirby amesema sasa kutakuwa na njia mbili kwa watu kutumia kuondoka maeneo hatari kaskazini mwa Gaza. Njia ya kwanza iliyofunguliwa siku chache zilizopita kwa muda wa saa nne na tano kila siku, tayari imewawezesha maelfu ya watu kufika maeneo salama mbali na maeneo ya mapigano.

Na njia ya pili kando ya Barabara ya pwani, itawezesha maelfu zaidi kufikia maeneo salama ya kusini”

Israel na Hamas wapambana karibu na hospitali mbili kwenye mji wa Gaza

Mara kwa mara Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amesisitiza kuwa hakutakuwa na usitishaji kamili wa vita bila kuachiliwa huru watu waliochukuliwa mateka na wanamgambo wa Hamas wakati wa shambulizi lao dhidi ya Israel la Oktoba 7.

Israel, Marekani na nchi kadhaa zimeliorodhesha kundi la Hamas kuwa la Kigaidi.