Waziri wa Ujerumani aonya juu ya ugaidi kanda ya Sahel
5 Machi 2024Matangazo
Shulze ametoa kauli hiyo wakati akianza ziara nchini Burkina Faso na Benin kwa mazungumzo ya kisiasa jana Jumatatu. Schulze amekuwa waziri wa kwanza barani Ulaya kuiziuru Burkina Faso tangu yalipotokea mapinduzi ya kijeshi mwezi Septemba mwaka 2022, yaliyomweka madarakani Ibrahim Traoré kuwa kiongozi wa taifa hilo. WaziriSchulze ni mwenyekiti wa muungano wa Sahel ulioundwa na Ujerumani, Ufaransa na Umoja wa Ulaya ili kuyasaidia mataifa ya ukanda huo wa Sahel. Ujerumani pia ndio mfadhili wa nne mkubwa wa muungano huo. Burkina Faso taifa lenye wakaazi takribani milioni 23, limekuwa chini ya mashambulizi ya makundi ya kigaidi kwa miaka kadhaa.