Waziri Mkuu wa zamani Pakistan Imran Khan akutwa na hatia
17 Januari 2025Mahakama nchini Pakistan imemuhukumu Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan kifungoo cha miaka 14 jela kwa kwa tuhuma za rushwa kuhusiana na uchunguzi wa awali wa utakatishaji fedha.
Khan, ambaye tayari yuko jela kufuatia mashtaka ya ufisadi, amekutwa na hatia ya rushwa na kutumia nafasi yake kama waziri mkuu kinyume cha sheria. Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Nasir Javed Rana kwenye mahakama iliyoundwa ndani ya gereza ambalo Khan anazuiliwa.
Soma: Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan ahukumiwa miaka 3 jela
Mwendesha mashtaka Muzaffar Abbasi aliwaambia waandishi wa habari baada ya hukumu hiyo kwamba mke wa Khan, ambaye pia anatuhumiwa kwenye kesi hiyo, alihukumiwa kifungo cha miaka saba kwa kumsaidia katika uhalifu.
Wakili wake Faisal Chaudhry amesema chama cha Khan kinanuia kupinga uamuzi huo katika mahakama ya juu zaidi kikidai imechochewa kisiasa.