1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer azuru Ujerumani

28 Agosti 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, anakutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Berlin hii leo Jumatano katika ziara yake ya kwanza tangu aingie madarakani mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/4k0E0
Ujerumani- Olaf Scholz -Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Justin Tallis/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, anakutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Berlin hii leo Jumatano katika ziara yake ya kwanza tangu aingie madarakani mwezi uliopita.

Viongozi hao watazungumza na waandishi wa habari baadae leo. Uingereza inapanga kuanzisha mazungumzo juu ya mkataba mpya wa ushirikiano na Ujerumani wakati inaangalia uwezekano wa kuanzisha upya uhusiano na Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uingereza amesema mkataba huo mpya ni sehemu ya juhudi za kuleta mwelekeo mpya katika mchakato wa Brexit. Mapema leo asubuhi Starmer alikutana na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.

Kiongozi huyo wa Uingereza baada ya mazungumzo yake mjini Berlin anatarajiwa kufanya ziara nchini Ufaransa ambako atakutana na Rais Emmanuel Macron ambako pia anatarajiwa kuhudhuria sherehe za ufungunguzi wa mashindano ya michezo ya Olimpiki kwa ajili ya watu wenye ulemavu mjini Paris.