Starmer afanya ziara Berlin kujadili mkataba na Ujerumani
28 Agosti 2024Hiyo ni ziara ya kwanza ya Keir Starmer nje ya nchi tangu alipoingia madarakani mwezi uliopita.
Uingereza inatarajiwa kufanya mazungumzo juu ya mkataba mpya wa ushirikiano na Ujerumani, wakati serikali ya chama cha Labour ikisaka kuhuisha uhusiano wake na Ulaya.
Soma pia: Starmer aitisha mkutano wa dharura kujadili ghasia
Starmer amesema mkataba huo ni sehemu ya jitihada za kuanza ukurasa mpya baada ya Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya Brexit.
Mkataba huo unahusisha sekta ya usalama wa nishati, teknolojia, sayansi na biashara. Baada ya Berlin, Waziri Mkuu wa Uingereza atasafiri kwenda Paris kukutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na akiwa huko, anatarajiwa kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya wanariadha walemavu.