1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Ugiriki Mitsotakis aapishwa muhula wa pili

26 Juni 2023

Waziri mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis ameapishwa kuongoza muhula wa pili madarakani baada ya chama chake cha New Democracy, kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa bunge

https://p.dw.com/p/4T4sr
Parlamentswahlen in Griechenland Alexis Tsipras
Picha: Michael Varaklas/AP Photo/picture alliance

Waziri mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis ameapishwa kuongoza muhula wa pili madarakani  baada ya chama chake cha New Democracy, kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa bunge. Waziri mkuu huyo amesema anataka kuanza mara moja utekelezaji wa mageuzi ya ziada huku akitarajiwa baadae leo kutangaza baraza lake la mawaziri.

Soma pia: Ugiriki yaingia katika duru ya pili ya uchaguzi

Chama chake kimeshinda asilimia 40.6 baada ya asilimia 99.6 ya kura kuhesabiwa kufuatia uchaguzi uliofanyika jana Jumapili.

Chama chake kimenyakuwa viti 158 kati ya viti 300 vya bunge na hivyo kumfanya kuwa na ushindi mkubwa wa moja kwa moja katika bunge hilo na kukifanya chama chake kuwa moja ya vyama vyenye nguvu kubwa katika Umoja wa Ulaya. Chama cha upinzani cha Syriza kimejipatia asilimia 17.8 ya kura, sawa sawa na viti 48 bungeni.