Ugiriki yaingia katika duru ya pili ya uchaguzi
25 Juni 2023Katika uchaguzi huu, Waziri mkuu Kyriakos Mitsotakis anatafuta kutetea kiti chake kwa muhula wa pili kupitia chama chake cha kihafidhina cha New Democracy (ND).
Soma Pia: Wahafidhina washinda uchaguzi nchini Ugiriki
Kwenye uchaguzi wa awali uliofanyika mwezi Mei, Mitsotakis alipata ushindi mkubwa lakini alikosa viti vitano vya wabunge ambavyo vingemuwezesha kuanzisha na serikali thabiti ya chama kimoja.
Licha ya kuwaomba wafuasi wake wajitokeze kwa wingi kwenye uchaguzi wa leo, Waziri huyo mkuu wa Ugiriki ametahadharisha kuwepo kwa uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi kwa mara ya tatu ikiwa atashindwa kupata kura za kutosha na viti vingi zaidi bungeni.
Mpinzani mkubwa wa Mitsotakis ni Waziri mkuu wa zamani Alexis Tsipras, aliyeshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa mwezi Mei.