1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Tunisia Najla Bouden atumbuliwa

3 Agosti 2023

Rais wa Tunisia Kais Saied amemfuta kazi waziri mkuu wa nchi hiyo, ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika taifa la Jumuiya ya Kiarabu.

https://p.dw.com/p/4UikK
Tunesien Regierungschefin Najla Bouden Ramadan
Picha: Yassine Mahjoub/NurPhoto/picture alliance

Shirika la habari la umma TAP limesema Najla Bouden ameachishwa kazi ya uwaziri mkuu na nafasi yake kuchukuliwa na Ahmed Hachani.

Hachani ambaye awali alifanya kazi katika Wizara ya Fedha ya Tunisia na benki kuu, aliapishwa na Saied Jumanne usiku.

Soma pia: Rais Saied amteua Waziri Mkuu mwanamke Tunisia

Hakukuwa na maelezo rasmi ya kufutwa kazi Bouden, ambaye wakosoaji walimuelezea kuwa ni "kivuli cha rais."

Lakini hatua hiyo inajiri wakati kukiwa na ongezeko la hali ya kutoridika nchini humo kuhusu uhaba wa chakula, kupanda kwa bei za bidhaa na mistari mirefu ya mara kwa mara ya kupata mkate, chakula ambao ni bidhaa muhimu nchini humo.