Rais wa Tunisia atangaza serikali mpya
11 Oktoba 2021Saied alimfuta kazi waziri mkuu, alisitisha vikao vya bunge na akajipa mamlaka ya kusimamia mahakama katika unyakuzi wa nguvu wa madaraka mnamo Julai 25 ambao wapinzani wameitaja hatua hiyo kama mapinduzi. soma zaidi Tunisia: Rais Kais Saied amfuta kazi Waziri Mkuu Hicham Mechichi
Serikali mpya inaongozwa na Najla Bouden, waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, ingawa Saied amejirudishia nguvu za ofisi hiyo na kwa utaalam ataongoza utawala mwenyewe. soma Rais wa Tunisia aahidi kutaja jina la waziri mkuu mpya
Najla Bouden
Rais alimteua Bouden, mtaalam wa jiolojia, mnamo Septemba 29, kama waziri mkuu zaidi ya miezi miwili baada ya kutengua utawala wa Hichem Mechichi na kuondoa kinga ya wabunge.
Bouden mwenye umri wa miaka 63, katika hotuba yake baada ya kuapishwa rasmi amesema vita dhidi ya ufisadi litakuwa lengo muhimu katika serikali mpya inayojumuisha wabunge 25.
Baraza jipya la mawaziri limetangazwa siku moja baada ya watu wasiopungua 6,000 kushiriki maandamano katikati mwa mji wa Tunis kupinga kile walichokiita unyakuzi wa madaraka wa rais Saied.
Baada ya hafla ya kuapishwa kwa serikali mpya raisi Saied alisema, "Mungu akipenda, tutafungua tena faili zote za ufisadi na hatutaondoa yoyote, hakuna anayependelewa kuliko mtu yeyote na hakuna nafasi kwa wanaotaka kuchanganya enzi kuu ya serikali na watu. Hatuko chini ya mamlaka ya mtu yeyote, lakini kadiri katiba inavyosema serikali, iliundwa na uundaji wake ulikuwa wa kasi zaidi kuliko wapinzani walivyotarajia." soma Rais Saied amteua Waziri Mkuu mwanamke Tunisia
Ushawishi wa Saied
Ingawa hatua ya Saied mnamo Julai 25 ilionekana kuwa maarufu baada ya miaka kadhaa ya kudorora kwa uchumi na kupooza kisiasa, upinzani dhidi yake umeanza kuimarika kwa kuandaa maandamano. Uteuzi wa serikali mpya kwa muda mrefu umekuwa ukishinikizwa na wanasiasa wa ndani na wafadhili wa nje, ambao pia wanashinikiza tamko ramsi kutoka kwa Saied juu ya muda wa kutatua mgogoro huo. soma Chama cha wafanyakazi Tunisia chaonya kuhusu demokrasia
Tunisia inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi katika mashirika yake ya umma huku shirika la fedha Duniani IMF awali liliashiria kwamba litajadiliana na serikali juu ya kujaribu kuikwamua kiuchumi lakini iwapo tu serikali itafanya mageuzi ya kuaminika katika mifumo yake.
Saied amesema hivi karibuni atatangaza mazungumzo ya kitaifa ambayo yatajumuisha makundi ya vijana kutoka kila pembe ya nchi hiyo, mazungumzo hayo yakijikita juu ya mustakabali wa Tunisia na mfumo wake wa kisiasa.
Vyanzo:AFP; Reuters