1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Italia aapa hatua kali kuzuia wahamiaji

Sylvia Mwehozi
16 Septemba 2023

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ameutolea mwito Umoja wa Ulaya kuchukua hatua za haraka za kuwazuia wahamiaji wanaovuka bahari ya Meditrenia wakitokea Afrika ya Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4WPWs
Lampedusa | Italien | Migranten
Picha: Yara Nardi/REUTERS

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ameutolea mwito Umoja wa Ulaya kuchukua hatua za haraka za kuwazuia wahamiaji wanaovuka bahari ya Meditrenia wakitokea Afrika ya Kaskazini.

Meloni ameapa hatua kali katika kushughulikia wimbi kubwa la wakimbizi waliowasili mnamo wiki hii katika kisiwa kidogo cha Lampedusa kilichotangaza kuzidiwa.Umoja wa Mataifa umesema wahamiaji karibu 7,000 walioingia katika kisiwa cha Lampedusa, Italia ni muhimu wakahamishwa

Waziri huyo mkuu, amesema kwamba amemwandikia rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel akiomba suala hilo la wakimbizi kuwekwa katika ajenda ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika mwezi Oktoba.

Serikali ya Meloni ya mrengo wa kulia iliingia madarakani mnamo mwezi Oktoba na kuapa kukabiliana na wimbi la wakimbizi. Lakini takribani wakimbizi 126, 000 wameripotiwa kuingia nchini Italia kwa kipindi cha mwaka huu, ikiwa ni mara mbili ya idadi kama hiyo mwaka uliopita.