1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Wazazi wasubiri hatma ya watoto shule iliyowaka moto Kenya

7 Septemba 2024

Familia za wanafunzi wa shule ya msingi nchini Kenya ambako bweni liliwaka moto usiku wa kuamkia jana Ijumaa na kuwaua watoto 17 wanasubiri kwa machungu taarifa za watoto wao ambao hadi sasa bado hawajapatikana.

https://p.dw.com/p/4kO3n
Shule iliyokumbwa na mkasa wa moto Kenya
Shule iliyokumbwa na mkasa wa moto Kenya. Picha: AP Photo/picture alliance

Hapo jana Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua akiwa kwenye eneo la mkasa huo aliwaambia waandishi habari kwamba wengine 70 waliokuwa shuleni hapa bado haijulikani walipo lakini alijizuia kusema juu ya iwapo walitetekea kwenye moto.

Janga hilo la moto kwenye shule ya msingi ya Hillside Endarasha iliyopo kwenye kaunti ya Nyeri lilitokea usiku wa manane kuamkia jana na kuliteketeza bweni lililokuwa na wanafunzi 150.

Rais William Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo ya taifa kuanzia Jumatazu inayokuja na ameutaja mkasa kuwa "janga lenye kutia machungu yasiyo mfano".