Watunisia wajitokeza kwa uchache kupiga kura
24 Desemba 2023Kulingana na Mamlaka Huru ya Uchaguzi nchini humo ISIE, wapiga kura wa Tunisia watachagua wawakilishi 2,000 kati ya wagombea 7,000 waliojitokeza kuomba ridhaa ya wananchi kuwawakilisha.
Uchaguzi huo utawezesha kuanzishwa kwa mabaraza ya mitaa, mikoa na wilaya na kuruhusu kuundwa kwa Bunge la pili.
Wapinzani wa Rais Saied wametoa wito wa kususia uchaguzi wa leo Jumapili na kuutaja kuwa sio halali.
Zaidi ya watu mashuhuri 260 nchini Tunisia walitia saini ombi la kupinga kile walichokiita "uchaguzi usiokuwa na maana," wakiamini kuwa serikali ya Saied inaendelea kutekeleza miradi yake ya kisiasa.
Tangu mapema mwaka huu mamlaka imewafunga jela zaidi ya wanachama 20 wa upinzani, akiwemo kiongozi wa Ennahdha Rached Ghannouchi na Jawhar Ben Mbarek, mwanzilishi mwenza wa chama cha National Salvation Front, miongoni mwa wengine.