Tunisia yawazuia karibu wakimbizi 2,500 kwenda Ulaya
20 Septemba 2023Matangazo
Msemaji wa Kikosi cha kitaifa cha Ulinzi Houssem Jbebli amesema jana kwamba hii ni baada ya operesheni ya siku nne iliyoendeshwa kati ya Septemba 15 na 18.
Amesema waliozuiwa ni pamoja na raia 581 wa Tunisia na wengine wakitokea kusini mwa jangwa la Sahara.
Vikosi vya usalama vya Tunisia vilianzisha operesheni katika maeneo mbalimbali ya pwani ambayo ni pamoja na Sfax, ambako idadi kubwa ya wahamiaji huanzia safari zao kwenda Italia.
Wiki iliyopita, Tunisia ilisema imeanzisha operesheni kubwa ya kusimamisha biashara haramu ya binaadamu na kuzuia idadi kubwa ya watu wanaokufa katika safari za mateso za baharini wakikimbilia Ulaya kutokea kwenye pwani zake.
Soma pia: