1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watatu wameuawa katika shambulio la jeshi la Israel.

22 Agosti 2024

Wizara ya afya inayodhibitiwa na kundi la Hamas imesema watu watatu wameuawa katika shambulio lililofanywa na Israel katika ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

https://p.dw.com/p/4jmTn
Uharibifu unaoshuhudiwa baada ya shambulio la Israel
Uharibifu unaoshuhudiwa baada ya shambulio la IsraelPicha: Ashraf Amra/picture alliance/Anadolu

Wizara hiyo imesema shambulio hilo limefanywa usiku wa kuamkia leo katika kambi ya wakimbizi ya Tulkarem. Hata hivyo, haijaelezwa iwapo waliouawa ni wapiganaji wa kundi la Hamas ama ni raia wa kawaida.

Jeshi la Israel limesema katika taarifa kuwa, shambulio lao la anga limelenga wapiganaji kadhaa katika kambi ya Tulkarem, huku jeshi likiendeleza oparesheni ya kutafuta vilipuzi vilivyozikwa ardhini katika eneo hilo.

Soma pia:Ukanda wa Gaza waendelea kushambuliwa na Israel

Eneo la Ukingo wa Magharibi limeshuhudia ongezeko la ghasia tangu shambulio la Hamas katika ardhi ya Israel mnamo Oktoba 7.