Watu watano wafariki Ujerumani mkesha wa mwaka mpya 2025
1 Januari 2025Matangazo
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini humo.
Msemaji wa polisi Florian Nath amesema maafisa 13 wa polisi wamejeruhiwa, akiwemo mmoja aliyepata majeraha mabaya.
Spma pia: Dunia yaikaribisha 2025 baada ya mwaka wa olimpiki, misukosuko na Trump
Watu 330 wamekamatwa katika mji mkuu Berlin usiku wa kuamkia leo huku taarifa ya polisi ikieleza kuwa, tofauti na miaka ya nyuma, mwaka huu mpya haukushuhudia matukio makubwa ya vurugu wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya.
Wajerumani husherehekea mwaka mpya kwa kurusha fashifashi, hali ambayo husababisha mijadala ya mara kwa mara juu ya kupiga marufuku fashifashi zinazoonekana kuwa hatari, hasa kutokana na idadi ya majeruhi kila mwaka, uchafuzi wa mazingira na kelele.