1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUhispania

Watu 9 wamefariki baada ya boti yao kuzama karibu na Canary

Saleh Mwanamilongo
28 Septemba 2024

Takriban watu tisa na wengine 48 hawajulikani waliko, baada ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji kuzama kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania.

https://p.dw.com/p/4lC6N
Shirika la uokoaji la kitaifa nchini Uhispania limesema watu 84 walikuwa ndani ya boti hiyo na 27 waliokolewa
Shirika la uokoaji la kitaifa nchini Uhispania limesema watu 84 walikuwa ndani ya boti hiyo na 27 waliokolewaPicha: Europa Press/AP Photo/picture alliance

Ajali hiyo inafuatia vifo vya wahamiaji 39 mwanzoni mwa Septemba wakati boti yao ilipozama kwenye ukanda wa pwani ya Senegal walipokuwa wakijaribu kuvuka hadi visiwa vya Canary, ambapo wahamiaji wanatarajia kuingia barani Ulaya.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, linakadiria kuwa watu 4,857 wamekufa kwenye njia hiyo hatari ya Bahari ya Atlantiki tangu 2014. Huku mashirika mengine ya misaada yakisema idadi hiyo ya Umoja wa Mataifa ni ndogo sana.