UhamiajiSenegal
Jeshi la wanamaji la Senegal laopoa miili 30
23 Septemba 2024Matangazo
Mamlaka za jeshi hilo zimeeleza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini sehemu ilikotoka meli hiyo na kuthibitisha idadi ya waliofariki.
Ukanda wa pwani wa Senegal unashuhudia vifo vya mara kwa mara vinavyohusisha majaribio ya wahamiaji kutaka kuingia Ulaya kwa kutumia mashua.
Mwezi Septemba, takriban watu 39 walifariki baada ya mashua yao kuzama karibu na mji wa bandari wa Mbour, magharibi mwa nchi hiyo.
Wakati rais wa Senegal Diomaye Faye akiahidi kukabiliana na magenge ya wahalifu yanayowasafirisha watu kimagendo, tangu kuanza kwa mwaka huu, wahamiaji 22,000 wamewasili kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania.