SiasaAsia
Watu 45,000 wakimbia makaazi yao Rakhine
24 Mei 2024Matangazo
Umoja wa Mataifa ulisema siku ya Ijumaa (Mei 24) kwamba wengi wa waathiriwa wanatoka jamii ya Waislamu wa Rohingya, huku kukiwa na madai ya watu kuuawa na mali kuchomwa moto.
Soma zaidi: Guterres "asikitishwa" na mauwaji Myanmar
Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva, msemaji wa Shirika la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, Elizabeth Throssell, alisema katika siku za hivi karibuni, makumi kwa maelfu ya raia wameyakimbia mapigano yanayoendelea katika viunga vya Buthidaung na Maungdaw.
Soma zaidi: UN yasikitishwa na mashambulizi ya anga yanayoendelea Myanmar
Throssell alisema kuwa Warohingya wanaokadiriwa kuwa 45,000 wameripotiwa kukimbilia eneo la Mto Naf karibu na mpaka wa Myanmar na Bangladesh wakitafuta usalama.