1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Watu 188 wafariki nchini Kenya kufuaria mafuriko

2 Mei 2024

Watu wasiopungua 188 wamekufa nchini Kenya kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi tangu mwezi Machi, huku wengine karibu 200,000 wakilazimika kuyahama makazi yao.

https://p.dw.com/p/4fRJm
Nairobi | Kenya | Hali ya Hewa | Mwanaume akiangalia athari za mafuriko.
Mwanaume akiangalia namna ambavyo mafuriko yamesababisha uharibifu katika eneo lake Kenya.Picha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Eneo la Afrika Mashariki limekumbwa na mvua kubwa zinazohusishwa na mfumo wa hali ya hewa wa El-Nino, na kusababisha mafuriko ambayo tayari yamepelekea vifo vya makumi ya watu na kuharibu nyumba za makazi, barabara, madaraja na miundombinu kadhaa.

Soma pia:Idadi ya vifo kufuatia mafuriko Kenya yafikia watu 181

Shirika la kimataifa la kutetea Haki za Binaadamu la Human Rights Watch limesema mamlaka za Kenya zimeshindwa kushughulikia kikamilifu athari za mafuriko hayo.

Lakini Rais William Ruto alitangaza kuwa watu wote wanaoishi katika maeneo yenye hatari ya kukumbwa na mafuriko watahamishiwa maeneo salama.