1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu 13 wauawa na wengine 113 wajeruhiwa Zaporizhzhia

9 Januari 2025

Shambulio la bomu lililorushwa na urusi lauwa watu wasiopungua 13 na wengine 113 wamejeruhiwa katika mji wa kusini mashariki mwa Ukraine wa Zaporizhzhia.

https://p.dw.com/p/4oyUo
Nchini Ukraine watu 13 wauawa na wengine 113 wajeruhiwa Zaporizhzhia kufuatia shambulio la Urusi
Nchini Ukraine watu 13 wauawa na wengine 113 wajeruhiwa Zaporizhzhia kufuatia shambulio la UrusiPicha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Mamlaka imesema miili kadhaa imetapakaa barabarani huku shughuli za usafiri wa umma zikiathirika.

Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine imesema kupitia mtandao wa Telegram kwamba majengo ya ghorofa, viwanda na miundombinu mengine imeharibiwa pia katika shambulio hilo.

Gavana wa eneo hilo, Ivan Fedorov amewaambia waandishi wa habari kuwa Urusi ilitumia mabomu mawili ya kurushwa kwa ndege yanayoongozwa kuelekea kwenye shabaha, kushambulia eneo hilo la maakazi ya watu.

Kulingana na gavana huyo, watu 10 kati ya 60 waliopelekwa hospitali wako katika hali mbaya na kuongeza kuwa, Alhamisi itakuwa siku rasmi ya maombolezo.