1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKenya

Watu 120 wamekufa kwa mafuriko nchini Kenya

29 Novemba 2023

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko yaliyokumba maeneo kadhaa nchini Kenya imefikia 120 huku maelfu ya makaazi yamesombwa na maji na kuwalazimisha watu kutafuta hifadhi.

https://p.dw.com/p/4ZYdR
Kenya Mombasa 2023 | Mafuriko
Mvua za El-Nino zimeleta mafuriko makubwa nchini Kenya na mataifa ya Pembe ya Afrika.Picha: REUTERS

Takwimu hizo mpya zimetolewa na afisa wa ngazi ya juu wa wizara ya mambo ya ndani ya Kenya, Raymond Omollo, ambaye pia amesema kaunti 4 za upande wa mashariki mwa nchi hiyo ndiyo zimeathirika zaidi na nyingine 10 zimo kwenye hali ya juu ya tahadhari.

Kulingana na afisa huyo, jumla ya nyumba 89,000 zimeharibiwa kwa mafuriko, hali iliyoilazimisha serikali kuanzisha kambi 112 za kuwahifadhi wale walipoteza maakaazi.

Mnamo siku ya Jumatatu, rais William Ruto aliongoza kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri kujadili athari za mafuriko na kuahidi kutoa mabilioni ya shilingi za Kenya kuwasaidia waliokumbwa na maafa.