Watoto 2,000 hufa kila siku kwa uchafuzi wa hewa - Ripoti
19 Juni 2024Matangazo
Taasisi hiyo inasema uchafuzi wa hewa ulichangia vifo vya watu milioni 8., ikiwa ni asilimia 12 ya vifo vyote vilivyotokea duniani katika mwaka wa 2021.
Zaidi ya vifo 500,000 katika hivyo vinadaiwa kusababishwa na matumizi ya nishati chafu ya kupikia kama mkaa, mbao au kinyesi cha ng'ombe na vilitokea hasa kwenye mabara ya Afrika na Asia.
Soma zaidi: WHO: Gaza bado inakabiliwa na kitisho cha njaa
Ripoti hiyo inasema uchafuzi wa hewa kwa sasa ndio sababu ya pili kubwa ya vifo vya mapema kote duniani.
Hii ina maana kwamba uchafuzi wa hewa sasa umevuuka matumizi ya tumbaku na ulaji mbaya na inashikilia nafasi ya pili baada ya shinikizo la damu kama sababu kuu ya kwanza ya vifo vya mapema duniani.