1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasifu wa Felix Tshisekedi

20 Desemba 2023

Felix Tshisekedi aliingia madarakani mwaka 2019 kupitia chama cha upinzani kilichoundwa na marehemu baba yake, Etienne Tshisekedi, aliyekuwa mpinzani mkubwa wa dikteta wa zamani, Mobutu Sese Seko.

https://p.dw.com/p/4aNdr
Rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili kuiongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili kuiongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Boniface Muthoni/SOPA Images/ZUMA/picture alliance

Felix, ambaye anatokea kabila la Luba kwenye wa jimbo la Kasai, alilazimika kumfuata baba yake huko akiwa na umri wa miaka 19 baada ya kupigwa marufuku kukanyaga mji mkuu, Kinshasa. 

Miaka mitatu baadaye, Mobutu alimruhusu Felix, ndugu zake na mama yao kwenda kuishi uhamishoni nchini Ubelgiji.

Soma zaidi: Je Felix Tshisekedi ni nani na ana mwelekeo upi?

Raia wa DRC wanajiandaa kumchagua rais wao

Kisha alianza kukwea kidogo kidogo ngazi za uongozi kwenye chama cha baba yake, UDPS, na mwaka 2011 alishinda ubunge kupitia kiti cha mji wa Mbuji-Mayi, mkoani Kisangani, lakini alikataa kuchukuwa ubunge huo kwa maelekezo ya baba yake, aliyemchukulia Joseph Kabila kuwa dikteta.

Etienne Tshisekedi alifariki dunia mwaka 2017, mwaka mmoja kabla ya mwanawe kuwania urais. 

Urais wa Tshisekedi

Mara tu baada ya kuingia madarakani, Felix Tshisekedi - ambaye sasa ana umri wa miaka 60 - alianza kujenga taswira yake mwenyewe na kufanya ziara nyingi za nje kinyume na mtangulizi wake, ambaye hakupenda kutembea.

Wafuasi wa Felix Tshisekedi wakiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa Disemba 20.
Wafuasi wa Felix Tshisekedi wakiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa Disemba 20.Picha: ARSENE MPIANA/AFP/Getty Images

Licha ya kuingia madarakani kwenye uchaguzi wenye utata ambao wengi wanaamini mshindi halisi alikuwa Martin Fayulu, Tshisekedi alivunja muungano wake wa kisiasa na Joseph Kabila anayetajwa kumsaidia kuingia madarakani na akaanzisha wake mwenyewe.

Soma zaidi: Wakongomani wapiga kura leo kuchagua viongozi wapya

Akifahamika kwa umashuhuri kwa jina la utani, "Fatshi" - ambalo ni ufupisho wa jina lake halisi - Tshisekedi ameiongoza Kongo kupita kipindi cha janga la UVIKO-19 na uasi unaoendelea wa kundi lam M23 kwenye eneo lenye utajiri wa madini la mashariki mwa nchi hiyo.

Ingawa kuna kiwango fulani cha ukuwaji wa uchumi, kiwango cha mfumuko wa bei na ukosefu wa ajira kinasalia kuwa cha juu mno kiasi cha kuchukuliwa kuwa jambo la kawaida katika taifa hilo lenye ufukara mkubwa.

Rais wa 'usiku'

Wafuasi wake wanamchukulia kuwa kiongozi madhubuti, ingawa kwa wapinzani wake, Tshisekedi ni kiongozi asiyekuwa na uwezo wa kuongoza na asiyestahiki kushikilia wadhifa huo.

Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: THOMAS PETER/REUTERS

Tshisekedi, mume na baba wa familia, anafahamika kuwa mtu anayezungumza taratibu na msikilizaji mzuri. Mmoja wa maafisa wake aliyefanya kazi naye kwa karibu, anamuelezea kama mtu mwenye kuwahishimu wengine na mwenye utu.

Soma zaidi: Rais Tshisekedi ana nadi sera zake Tanganyika

Rais huyo pia ana sifa ya mtu anayechelewa kuamka, anayeongoza nchi usiku. Hotuba zake za usiku mkubwa ni jambo la kawaida, na maafisa wengi waliliambia shirika la habari la AFP kwamba mikutano mikubwa ya serikali mara nyingi hufanyika usiku wa manane.

Vyanzo: AFP, Reuters