Tshisekedi kuwasili mara ya kwanza Tanganyika tangu uchaguzi
7 Desemba 2023Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi atanadi sera zake jimboni Tanganyika ikiwa ni mara ya kwanza kuingia jimboni humo tangu alipochaguliwe kuwa kiongozi wa nchi hiyo.
Rais Felix Tshisekedi atawasili jioni (07.12.2023) jimboni humu ikiwa ni mara ya kwanza toka aingie madarakani. Rais Tshisekedi anawania urais kupitia chama tawala cha UDPS huku akiungwa mkono na vyama vingine vidogo vyenye kuunda muungano wa Union Sacré nchini humo.
Hamasa ya raia ya kumsikiliza mgombea Tshisekedi
Maelfu ya raia wanamsubiri kwa hamu kiongozi huyo wa nchi, huku wakiwa na shauku ya kumuona kwa mara ya kwanza, wakitegemea kupata hotuba itakayosaidia kuboredha maisha yao. Jimbo la Tanganyika ni miongoni mwa majimbo nchini humu yenye usalama mdogo.
Soma zaidi:Upinzani Kongo kuafikiana juu ya kusimamisha mgombea mmoja?
Kwa upande wake, mchambuzi wa masuala ya kisiasa Kalinde Bavon, amebainisha kuwa ujio wa Rais Tshisekedi utawasaidia raia kujua maendeleo ya nchi yao endapo atachaguliwa tena.
DW Kalemie, Kongo.