Washington: Rais Bush wa Marekani na rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Barroso, wazungumza juu ya tafauti katika masuala baina ya biashara baina ya pande zao mbili.
9 Januari 2007Matangazo
Rais George Bush wa Marekani na Rais wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso, wamesema Marekani na Umoja wa Ulaya zinahitaji kutanzua tafauti zao juu ya masuala ya siasa za biashara ikiwa zinataka kuyaanzisha tena mazungumzo yaliokwama kuhusu biashara ya dunia. Baada ya mkutano wao katika Ikulu ya Marekani, Bwana Barroso alisema mazungumzo ya Doha yamefikia njia panda. Mazungumzo hayo yamekwama kutokana na suala kwa kiwango gani Umoja wa Ulaya na Marekani zipunguze ruruku zinazotoa kwa wakulima wao katika juhudi za kuyapa mataifa maskini nafasi ilio bora ya kushindana katika masoko ya dunia.