MigogoroAfrika
Washambuliaji wawaua watu 15 Sudan Kusini
21 Machi 2024Matangazo
Waziri wa habari wa mkoa huo Abraham Kelang, alisema kuwa vijana wanaoshukiwa kuwa na silaha kutoka kabila la Anyuak kwenye kaunti ya Pochalla, waliuvamia msafara huo siku ya Jumanne.
Sababu ya shambulio hilo haikufahamika mara moja, lakini Kelang alimshutumu kamishna wa zamani ambaye alitimuliwa kutoka wadhifa wake katika kaunti ya Pochalla kwa kuwachochea vijana wa Anyuak.
Mapigano kati ya makundi hasimu ya kikabila nchini Sudan Kusini huzuka mara kwa mara, mara nyingi yakichochewa na wizi wa ng'ombe na mizozo juu ya maliasili au ulipaji kisasi wa mashambulizi yaliyopita. Jamii nyingi zinazozozana nchini Sudan Kusini zimejihami kwa silaha, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano mwaka 2013.