Warohingya wakumbuka miaka sita ya mauaji ya halaiki
25 Agosti 2023Wakimbizi hao wanataka haki itendeke kufuatia kamatakamata na mauaji yaliyofanywa na jeshi la Myanmar dhidi yao miaka sita iliyopita.
Kiongozi wao, Mohammad Jubair, aliliambia kundi la wakimbizi katika kambi ya Kutupalong kwamba jamii ya kimataifa haijawatendea haki.
Soma zaidi: Watu 6 wauwawa katika makabiliano kwenye kambi ya wakimbizi Bangladesh
Warohingya Bangladesh huenda wakakabiliwa na utapiamlo
Shirika la amani na haki za binaadamu la Arakan Rohingya ndilo lililoandaa maandamano hayo katika kambi 34 za wakimbizi, ambazo ni makao ya zaidi ya Warohingya milioni moja waliokimbia mateso nchini kwao, Myanmar.
Myanmar haiwatambui sehemu kubwa ya jamii hiyo ya Waislamu, linalotajwa kuwa kundi kubwa la watu duniani lisilotambuliwa uraia wao na taifa lolote.