SiasaBangladesh
Warohingya Bangladesh huenda wakakabiliwa na utapiamlo
3 Machi 2023Matangazo
Hii ni baada ya hatua iliyoanza kutekelezwa mwezi huu ya wafadhili wa kimataifa kupunguza msaada wa chakula. Siku ya Jumatano, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilipunguza mgao huo kwa asilimia 17.
MSF imetoa wito kwa wafadhili kutoa kipaumbele kwa wakimbizi wa Rohingya wanaoishi katika mazingira duni kwenye kisiwa kilichopo kwenye Ghuba ya Bengal, na kuthibitisha ahadi zao za ufadhili. Bangladesh imewapokea zaidi ya Waislamu milioni 1 wa Rohingya ambao
walikimbia mateso katika nchi jirani ya Myanmar.