Argentina yafanya uchaguzi katikati ya mdororo wa kiuchumi
19 Novemba 2023Uchaguzi huo aidha unakabiliwa na kinyang'anyiro kikali kati ya Waziri wa Uchumi Sergio Massa na mwanauchumi Javier Milei.
Wagombea hao wawili wana mitizamo tofauti juu ya mustakabali wa uchumi wa taifa hilo la tatu kwa ukubwa barani Amerika ya Kusini, unaokabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei, kufuatia madeni ya muda mrefu, usimamizi mbaya wa fedha na kuyumba kwa sarafu.
Kura zilianza kupigwa majira ya saa 2:00 asubuhi kwa saa za nchini humo na zitafungwa saa 12:00 jioni, huku matokeo yakitarajiwa muda mfupi baada ya kufungwa kwa vituo.
Massa, 51, ni mwanasiasa mwenye haiba na mzoefu anayetaka kuwashawishi Waajentina kumwamini licha ya utendaji wake kama waziri wa uchumi ulioshuhudia mfumuko wa bei wa kila mwaka ukifikia asilimia 143 na rekodi ya juu ya viwango vya umaskini.
Mpinzani wake ameahidi pamoja na mambo mengine kusitisha matumizi yasiyodhibitiwa ya Argentina