Wapiga kura nchini Mali waidhinisha mabadiliko ya katiba
24 Juni 2023Matangazo
Maafisa wa uchaguzi wamesema idadi ya wapiga kura katika kuamua mabadiliko hayo mnamo Jumapili iliyopita ilikuwa chini ya asilimia 39.4 ya watu milioni 8.4 waliojiandikisha kupiga kura.
Soma zaidi:Mali wapigia kura rasimu mpya ya katiba
Uongozi wa kijeshi nchini humo na mamlaka za kikanda ambao kwa pamoja waliunga mkono kura hiyo ya maoni wamesema hatua hiyo itaiwezesha Mali kufanya uchaguzi Februari 24 mwakani na kurejea kwenye utawala wa kiraia. Hata hivyo, wapinzani wanasema mabadiliko hayo yatawezesha jeshi kusalia madarakani baada ya uchaguzi mwaka ujao.