SiasaMali
Mali wapigia kura rasimu mpya ya katiba
18 Juni 2023Matangazo
Utawala wa kijeshi nchini humo umesema kura hiyo inaanzisha mchakato wa mpito wa kurejeshwa kwa utawala wa kiraia. Uchaguzi wa bunge umepangwa kufanyika mwezi Oktoba na ule wa urais utafanyika mwezi Februari.
Hata hivyo kura ya leo ya kuamua juu ya katiba mpya ilicheleweshwa kwa miezi mitatu huku wasiwasi ukisalia bado, ikiwa utawala wa kijeshi utaheshimu mchakato huo.
Chini ya katiba mpya inayopendekezwa itakayochukua nafasi ya katiba ya mwaka 1992, jukumu la rais na jeshi vitapewa mamlaka makubwa kupitia bunge.