1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Ujerumani wawasili Lithuania kwa mara ya kwanza

8 Aprili 2024

Viongozi wa Lithuania wameisifu hatua ya kihistoria ya Ujerumani ya kuanza kupeleka wanajeshi katika taifa hilo la Baltiki na mwanachana wa NATO.

https://p.dw.com/p/4eYQC
Deutschland | Verteidigungsminister Pistorius verabschiedet Brigade Litauen
Picha: Lisi Niesner/REUTERS

Hi ni mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, ambapo wanajeshi wa Ujerumani wataweka kambi ya muda mrefu nje ya nchi.

Karibu wanajeshi 24 wamewasili Lithuania, tayari kuandaa mazingira ya wengine 150 wanaotarajaiwa kuungana nao baadae mwaka huu. Jumla ya wanajeshi 5,000 wanatarajiwa kukita kambi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027.

Waziri wa Ulinzi wa ujerumani Boris Pistorius amezungumzia hatua hiyo mjini Berlin alipokuwa akiwaanga wanajeshi hao akisema hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kuwa na kikosi cha kudumu nje ya nchi na kuiita siku hii kuwa ni muhimu kwa jeshi la Ujerumani.

Waziri wa ulinzi wa Lithuania Laurynas Kasciunas kwa upande wake ameisifu hatua hiyo kuwa ni mfano mkubwa kwa nchi zote wanachama NATO katika upande wa mashariki kwenye mpaka na Urusi na mshirika wake, Belarus.