1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati nchini Kenya wapinga ongezeko jipya la kodi

18 Juni 2024

Raia nchini Kenya walikusanyika nje ya jengo la bunge hii leo kupinga ongezeko la kodi zenye utata, huku polisi wakipambana nao kwa gesi ya kutoa machozi na kuwakamata karibu watu watatu.

https://p.dw.com/p/4hBf0
Wanaharakati Kenya wapinga mswada wa fedha wa mwaka 2024 nchini humo
Wanaharakati Kenya wapinga mswada wa fedha wa mwaka 2024 nchini humoPicha: YASUYOSHI CHIBA/AFP

Polisi wamepambana na waandamanaji kwa kutumia gesi ya kutoa machozi na kuwakamata karibu watu watatu. Taarifa hii ni kulingana na waandishi wa AFP waliokuwa eneo la tukio.

Taarifa za maandamano hayo yaliyopewa jina "Vamia Bunge" zilisambazwa mitandaoni baada ya wanaharakati kuvujisha mawasiliano ya wabunge na kuwataka watu kuwapigia simu na kuwatumia ujumbe wa kuwashinikiza kukataa muswada unaopendekeza ongezeko jipya.  

Taifa hilo lenye nguvu kubwa kiuchumi Afrika Mashariki limekuwa likikabiliwa na mzozo wa ongezeko la gharama za maisha, ambao wakosoaji wanasema utaongezeka kutokana na mapendekezo hayo ya kodi.

Miongoni mwa miswada inayopingwa zaidi ni wa kodi ya magari unaopangwa kuongezwa kwa asilimia 2.5 ya thamani ya gari na kurejeshwa kwa Kodi ya Ongezeko kwenye mkate.